Follow by Email

Friday, March 15, 2019

Tanzania na Brazil kuendelea kuimarisha ushirikiano

Bw. Jestas A. Nyamanga, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisalimiana na Mhe. Antonio Augusto Martins Cesar, Balozi mpya wa Brazil hapa nchini walipokutana kwa mazungumzo kwenye ofisi ndogo za Wizara zilizopo Dar es Salaam hivi karibuni. Pamoja na mambo mengine, mazungumzo yao yalijikita katika kuimarisha uhusiano baina ya Tanzania na Brazil hususan katika  sekta ya afya, kilimo biashara na uwekezaji wa viwanda. Kwa upande wake, Mhe. Balozi Cesar aliahidi kutoa ushirikiano kwa Wizara na Serikali kwa ujumla ili kuhakikisha uhusiano baina ya Tanzania na Brazil unafikia malengo yaliyokusudiwa kwa maslahi ya mataifa haya mawili. 
  Bw. Nyamanga akimweleza jambo Mhe. Cesar, Balozi wa Brazil hapa nchini wakati wa mazungumzo yao. No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.