Follow by Email

Friday, July 19, 2019

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga Balozi wa Switzerland na Denmark waliyomaliza muda wa kazi nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Balozi wa Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli zawadi ya picha ya kuchora ya  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akimkabidhi Balozi Jensen zawadi ya picha iliyochorwa  Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro kama kumbukumbu yake ya vivutio vya utalii vilivyopo Tanzania
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akizungumza wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na Wizara kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen na Balozi wa Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli hapa nchini ambao wamemaliza muda wao wa kazi. Hafla hiyo ilifanyika kwenye Hoteli ya Hyatty Regency Jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen (wa pili kutoka kulia), Balozi wa Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Uingereza Mhe. Sarah Cooke na Kaimu Balozi wa Marekani Bi. Inmi Petterson kwa pamoja wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Balozi wa Italy Mhe. Roberto Mengoni (wa kwanza kushoto) na Katibu wa Waziri Bw. Charles Mbando wakimsikiliza kwa makini Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)
Switzerland Mhe. Florence  Tinguely Mattli naye alitoa neno la shukrani kwa ushirikiano alioupata wakati wote wa utekelezaji wa majukumu yake akiwa hapa nchini. ambapo ameahidi kuendelea kushirikiana na kuitangaza vyema Tanzania 
Balozi wa Denmark Mhe. Einar Hebogard Jensen naye alishukuru kwa ushirikiano alioupata wakati wote katika kutekeleza majukumu yake akiwa hapa nchini. Hata hivyo hakusita kumpongeza Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kwa jitihada zake za kupambana na Rushwa pamoja na kujenga miundombinu mizuri hapa nchini.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Pof. Palamagamba John Kabudi (katikati), kiongozi wa Mabalozi nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoul Mohamed (wakwanza kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Jestas Nyamanga wakiwasikiliza Balozi wa Sweden na Denmark (hawapo pichani) walipokuwa wakizungumza.
Kiongozi wa Mabalozi nchini Tanzania Mhe. Dkt. Ahamada El Badaoul Mohamed naye akizungumza neno wakati wa hafla ya kuwaaga Mabalozi wa Switzerland na Denmark (hawapo pichani)  Dkt. Ndumbaro azungumza na Mkuu wa Timu ya kujitegemea ya Umoja wa Mataifa Bw. Youssef Mahmoud.


Prof. Kabudi apokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule nchini

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) akipokea nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa India, Mhe. Sanjiv Kohli. Hafla hiyo ilifanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam.
Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb) akizungumza na Balozi mteule Sanjiv Kohli mara baada ya kupokea nakala zake
Mazungumzo yakiendelea
Prof. Palamagamba John Kabudi akiagana na Balozi Mteule Mhe. Sanjiv Kohli mara baada ya kumalizaka kwa hafla hiyo
Ubalozi wa Tanzania nchini India wafanikisha hafla ya uzinduzi wa safari za Air Tanzania mjini Mumbai

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwele akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa safari za  Shirika la Ndege la Tanzania (Air Tanzania) katika mji wa Mumbai nchini India. Uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Bandra Kurla mjini Mumbai tarehe 18 Julai 2019
Waziri wa Elimu, Michezo na Ustawi wa Vijana wa India ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi rasmi wa safari za a Shirika la Ndege la Tanzania mjini Mumbai nae akizungumza kwenye hafla hiyo
Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda akitoa neno la ukaribisho kwa wageni waalikwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za ndege za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai nchini India
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Ndege ya Tanzania, Mhandisi Emmanuel Korosso nae akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa safari za Air Tanzania mjini Mumbai, India
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akiwa tayari kukata utepe kuashiria kuanza rasmi kwa safari za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai, India
Mhe. Kamwele akiwa na Viongozi wengine kutoka Tanzania na India wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa safari za Shirika la Air Tanzania mjini Mumbai
Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akikata keki maalum kuashiria kuanza rasmi kwa safari za Ndege za Air Tanzania mjini Mumbai, India
Matukio mbalmbali ya ushirikiano kati ya Tanzania na India wakati wa uzinduzi wa safari za ndege za Air Tanzania mjini Mumbai
Mhe. Waziri Kamwelwe akipokea Jarida la Travel ambalo ambalo huandika taarifa kuhusu masuala ya usafirishaji na uchukuzi kwa ujumla
Mhe. Waziri Kamwelwe (wa pili kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Baraka Luvanda (wa tatu kushoto), viongozi mbalimbali kutoka Tanzania na India pamoja na Marubani waliofamikisha ndege ya kwanza ya Air Tanzania kutua Mumbai kwa ajili ya safari za kibiashara 
Mhe. Balozi Luvanda katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki uzinduzi wa safari za ndege ya Air Tanzania mjini Mumbai. Kushoto ni Bw. Kheri Goloka, Afisa wa Ubalozi Mwandamizi.

Wafanyabiasha kutoka China ziarani nchini kutafuta fursa za biasharaTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wafanyabiashara kutoka Jimbo la Zhejiang, China kuja nchini kutafuta fursa za biashara

Ujumbe wa wafanyabiashara 25 kutoka Kampuni kubwa 15 za Jimbo la Zhejiang nchini China ukiongozwa na Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Bunge la Jimbo hilo, Mhe. Bi. GE Huijun utafanya ziara nchini kuanzia tarehe 20 hadi 23 Julai 2019 kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali kuhusu fursa za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.

Ziara hiyo inalenga kukuza mahusiano ya kiuchumi baina ya Jimbo la Zhejiang na Tanzania katika sekta mbalimbali za maendeleo kama vile teknolojia, mawasiliano, ujenzi na uchukuzi, afya na madini.

Mhe. GE Huijun pia atafuatana na viongozi 13 wa Serikali ya Zhejiang kwenye ziara hiyo ambayo itaanzia Zanzibar tarehe 20 Julai 2019.

Ujumbe huo ukiwa nchini, pamoja na masuala mengine, unategemea kukutana na Viongozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar kwa ajili ya kujadiliana nao kuhusu fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo nchini.

Ukiwa Zanzibar, ujumbe huo utatembelea maeneo ya viwanda ya Amani na Fumba kwa ajili ya kujionea fursa za uwekezaji. Aidha, ujumbe huo utakutana na Mamlaka ya Uwekezaji na Uendelezaji Vitega Uchumi Zanzibar (ZIPA) pamoja na kukutana na wafanyabiashara wa Zanzibar kwa madhumuni ya kuanzisha ushirikiano.

Kadhalika ujumbe huo utashiriki ufunguzi wa Kongamano la Biashara kati ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Wafanyabiashara kutoka Zhejiang utakaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 22 Julai 2019.

Ujumbe huo unategemea kukamilisha ziara yao nchini tarehe 23 Julai, 2019.


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
19 Julai 2019


Thursday, July 18, 2019

VACANCY ANNOUNCEMENT


PRESS RELEASE

VACANCY ANNOUNCEMENT FROM THE INTERNATIONAL TELECOMMUNICATION UNION (ITU)

The Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation has received Vacancy Notice No. 21D-2019/BDT-DDR/External/D2 from the International Telecommunication Union (ITU) inviting qualified Tanzanians to apply for the post of  Deputy to the Director and Chief of the Administration and Operations Coordination Department (DDR).

Application details can be found through the ITU website: http://www.itu.int/employment/Recruitment/index.html.

Closing date for application is Sunday 25th August 2019.


Issued by;
Government Communication Unit,
Ministry of Foreign Affairs and East African Cooperation,
Dodoma.
18th July 2019.


Wednesday, July 17, 2019

Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Nchi za SADC


Prof. Kabudi azungumza na Mabalozi wastaafu wa Tanzania

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani kwa nia ya kupata ushauri na maoni yao kuhusu maandalizi ya Mkutano wa 39 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC). Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Julius Nyerere uliopo jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huo Prof. Palamagamba John Kabudi ameongozana na Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe (wa kwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi (wa kwanza kulia).  
Juu na Chini ni sehemu ya Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani wakimsikiliza Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani). 


Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani) 
Mkutano ukiendelea
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.), Naibu Waziri Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro (Mb.), Katibu Mkuu Dkt. Faraji Kasidi Mnyepe, Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakiwa katika picha ya pamoja na Mabalozi wastaafu walioiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali duniani Tuesday, July 16, 2019

Prof. Kabudi akutana na Mabalozi wa Nchi za SADCWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) waliopo hapa nchini.


Katika mazungumzo hayo Prof. Palamagaba John Kabudi amewafahamisha hatua iliyofikiwa katika maandalizi ya Mkutanao ya wakuu wa nchi na Serikali wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliyopangwa kufanyika nchini mwezi Agosti 2019 Kwa upande wa waheshimiwa Mabalozi hao walifurahishwa kwa hatua ya maandalizi iliyofikiwa, na kuelezea furaha yao kuhusu uwamuzi wa Serikali kuwashirikisha mapema katika maandalizi hayo.


Sehemu ya Mabalozi wa Nchi za Afrika na wanachama wa Jumuiya ya SADC wakimsikiliza Prof. Palamagamba John Kabudi (hayupo pichani)

Sehemu nyingine ya watumishi kutoka Balozi za Afrika zilizopo nchini
Prof. Palamagamba John Kabudi akifafanua jambo kwa Waheshimiwa Mabalozi alipokutana nao
Balozi wa Afrika Kusini Mhe. Thamsanga Mseleku akielezea jambo katika mkutano na Waziri Prof. Palamagamba John Kabudi Mkutano ukiendelea.
Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech watua nchini kutafuta fursa za biashara na uwekezajiTAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech watafuta fursa za biashara na uwekezaji nchini Tanzania

Ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech wamewasili nchini tarehe 13 Julai, 2019 kwa lengo la kukutana na kufanya mazungumzo na wadau mbalimbali nchini ili kujadili fursa za biashara na uwekezaji nchini katika sekta mbalimbali hususan afya, kilimo, miundombinu ya barabara na reli,nishati, madini,utalii na wa ujenzi wa viwanda vya madawa na vifaa tiba.

Ziara hiyo inatokana na juhudi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kupitia Ubalozi wa Tanzania uliopo nchini Ujerumani ambao pia unawakilisha Tanzania katika Jamhuri ya Czech na wadau wengine muhimu katika kushawishi wafanyabiashara wakubwa kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali.

Ujumbe huo wa watu kumi na mbili (12) ukiwa nchini, pamoja na masuala mengine, unategemea kukutana na uongozi wa Wizara naTaasisi mbalimbali zikiwemo, Wizara ya Viwanda na Biashara, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Wizara ya Nishati, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bohari Kuu ya Dawa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam. 

Vilevile, ujumbe huo unategemea kushiriki katika Kongamano la Uwekezaji wa Viwanda vya Kutengeneza Madawa na Vifaa Tiba kwa ubia kati ya Serikali na Sekta Binafsi, lililoandaliwa na Bohari Kuu ya Dawa. Kongamano hilo limepangwa kufanyika tarehe 17 Julai, 2019 katika Ukumbi wa Mkutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Ziara ya ujumbe huo nchini ni chachu ya kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Czech. Kadhalika, ziara ya ujumbe huo ni moja ya mikakati ya utekelezaji wa Sera ya Mambo ya Nje inayojikita katika diplomasia ya uchumi na kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda ili kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.

Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Tanzania asiye na makazi nchini Czech ameambatana na ujumbe huo wa wafanyabiashara na wawekezaji.

Ujumbe huo kutoka Jamhuri ya Czech unategemea kukamilisha ziara yao nchini tarehe 17 Julai, 2019.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.

16 Julai 2019


Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ambaye pia ni Balozi wa Tanzania asiye na makazi nchini Czech akiwa kwenye mkutano kati ya ujumbe wa wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech na Kituo cha UwekezajiTanzania (TIC) uliofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 15 Julai 2019. Mhe. Balozi Possi ameambatana na ujumbe huo hapa nchini ambao una lengo la kutafuta fursa za biashara na uwekezaji kwenye sekta za afya, kilimo, nishati na madini na ujenzi wa viwanda vya madawa na vifaa tiba.
Sehemu ya Wafanyabiashara na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech ukufuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa kwao na Wataalam kutoka Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC)
Sehemu nyingine ya Wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech 
Mkutano ukiendelea
Mhe. Balozi Possi (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi wa TIC na wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Jamhuri ya Czech.

Friday, July 12, 2019

MASHINE YA KWANZA INAYOPIMA UDONGO NA KUKUAMBIA KIASI CHA MAZAO UTAKACHOPATA


Maabara ya kisasa ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalum yazinduliwa

Makamu Waziri wa Uholanzi Bi. Marjolijn Sonnema (watatu kushoto) na Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega(watatu kulia) akikata utepe kuashilia uzinduzi wa Teknolojia ya Maaabara ya kupima afya udongo kwa kutumia gari maalum uliofanyika Jijini Arusha hivi karibuni. kushoo ni Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania Joroen Verheul, wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT centre ltd Bw.Geoffrey Kirenga, wa pili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na kulia ni Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dkt.Edmond Matafu ambaye ndie mwekezaji wa teknolojia hiyo nchini.
Mkurugeni Mkuu wa Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) Dk. Edmond Matafu (kulia) akitoa maelekezo ya namna Maabara ya kupima afya ya udongo inavyofanya kazi kwa Makamu Waziri wa Uholanzi Bi.Marjolijn Sonnema(wapili kulia) mara baada ya kuzindua maabara hiyo inayotumia gari maalum hivi
karibuni jiijini Arusha. Wapili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SAGCOT Centre Ltd, Geoffrey Kirenga.
Gari Maalum yenye maabara ya kupima afya ya udongo limezinduliwa hvi karibuni jijini Arusha. Kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) ndiyo itakayoendesha zoezi la kupima afya ya udongo katika mashamba ya wakulima kote nchini kwa gharama ya shilingi 25,000 mpaka 30,000.
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akipeana mkono na Dk. Edmond Matafu, ambaye ni moja wa wawekezaji walioleta maabara hiyo ambayo itaidia sana wakulima kwani watakuwa wanapima udongo huo kabla ya kulima. 
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega, akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo. 
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Kilimo Maliasili na Usalama wa Chakula Bi. Marjolyn kutoka nchini Uholanzi, pamoja na Dk. Edmond Matafu, wakikata utepe ikiwa ni ishara ya maabara hiyo ya kutembea imezinduliwa rasmi. 
Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega akizungumza jambo mara baada ya kuzindua maabara hiyo ya upimaji wa udongo.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo maliasili na Usalama wa Chakula Bi Marjolyn kutoka nchini Uholanzi wakikata utepe ishara ya kufungua rasmi maabara za utupimaji wa udongo. (Picha zote na Ahmed Mahmoud, Arusha).


Na Mwandsihi Wetu, Arusha

TEKNOLOJIA ya maabara ya kupima afya ya udongo kwa kutumia gari maalumu lenye uwezo kupima zaidi ya sampuli 100 za udongo kwa siku moja limezinduliwa hapa nchini ili kupima udongo na kumhakikishia mkulima uzalishaji wa mazao kwa wingi na yenye tija sokoni.Uzinduzi wa Teknolojia hiyo kutoka nchini Uholanzi ulifanyika jijini Arusha kati ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bw.Abdallah Ulega kwa niaba ya Tanzania na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula wa Uholanzi, Bi.Marjolijn Sonnema kwa niaba ya nchi yake ili kufanikisha mageuzi katika sekta ya kilimo.

Akizungumza mara baada ya kufanya uzinduzi wa teknolojia hiyo, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Bw Ulega aliishukuru Serikali ya Uholanzi kwa kutoa teknolojia yake kwa Tanzania na kusema kuwa itasaidia kuleta mapinduzi katika uzalishaji mazao.

“Kupima afya ya udongo inatoa majibu juu ya ubora wa ardhi husika, mazao yanayofaa kulimwa katika eneo hilo, kiwango cha mbolea kinachotakiwa na kutoa makadirio ya kiwango cha mavuno katika eneo husika,” alisema Naibu Waziri Ulega.

Aliongezea kuwa gharama ya kupima shamba iliyowekwa ya shilingi 25,000 mpaka 30,000 wakulima wanaweza kumudu na kuwataka wapema mashamba yao kabla ya kufanya kilimo ili kujua matatizo yaliyopo kwenye ardhi yake na nini afanye ili tija ya uzalishaji iongezeke.

“Teknolojia hii imeletwa kwetu hivyo tunakila sababu ya kuhamasisha wakulima nchini kupima mashamba yao ili wajipatie uhakika wa zao lilalofaa katika ardhi yake na nini afanye katika kuboresha ili aweze kuongeza tija ya uzalishaji,” alisema.

Naibu Waziri Ulega aliesema kuwa mageuzi katika sekta ya kilimo yatapatikana kupitia teknolojia hii ya kupima afya ya udongo na kupelekea kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya kilimo hali itakayochochea ujenzi wa viwanda vya kuchakata na kuongezea thamani ya mazao.

“Ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi kunachochea kasi ya maendeleo kwa kuibua teknolojia na ujuzi mbalimbali katika kuiletea nchi maendeleo, naipongeza kampuni ya Life Support System Tanzania (LSSL) kwa kuwekeza kwenye ketnolojia hii,” alisema Ulega Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa LSSL, Dkt.Edmond Matafu alisema magari manne yapo tayari pamoja na handheld soil scanner 100 ambazo zitatumiwa na maafisa ugani kwa ajili ya kuchukua sampuli za udongo katika maeneo ya vijiji kote nchini.

“Hii itasaidia kufanya zoezi la kupima afya ya udongo kwa wakati pasipo kuchelewa kipindi cha kulima ambapo itampa unafuu mkulima kujua mahitaji katika shamba lake ili aweze kupata tija katika uzalishaji mazao,” alisema Dkt. Matafu.

Aliongezea kuwa juhudi za Serikali za kujenga uchumi wa kati na viwanda zitatekelezeka kwa ushirikiano kati ya sekta binafsi na Serikali kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha vikwazo vyote vinavyokwamisha maendeleo vinatatuliwa ili maendeleo tunayoyatarajia yaweze kufikiwa kwa vitendo.

“Zoezi la kupima afya ya udongo litafanyika kote nchini kwani tumejipanga vizuri katika kutoa huduma hii kwa wakulima hivyo ushirikiano ndio kitu muhimu katika kufanikisha zoezi hili ambalo litakwenda kuinua hali ya uzalishaji zao nchini,” alisema Dkt. Matafu.

Uzinduzi wa Maabara ya kupima udongo kwa kutumia gari maalum ulishuhudiwa na Makamu Waziri wa Kilimo na Ubora wa Chakula kutoka Uholanzi, Bi. Marjolijn Sonnema, Balozi wa Uholanzi nchini Tanzania

Joroen Verheul, Katibu Mkuu Wizara ya Mifungo na Uvuvi Profesa Elisante Ole Gabriel na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe na Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Kuendeleza Kilimo Nyanda za Juu Kusini, Bw. Geoffrey Kirenga.