Follow by Email

Wednesday, September 26, 2018

Prince William awasili nchini

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt Hamis Kigwangala(Mb.), akisalimiana na Mjukuu wa Malkia "Prince" William mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku nne nchini.  “Prince” William akiwa nchini pamoja na mambo mengine atafanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli. Aidha, atatembelea kikosi cha Maji cha Jeshi la Polisi; Bandari ya Dar es Salaam; Jengo la Wizara ya Maliasili na Utalii (Mpingo House); Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi iliyopo mkoani Tanga na Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori cha Mweka kilichopo mkoani Kilimanjaro.
"Prince" William akisalimiana na Waziri wa Sheria na Katiba Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi (Mb.) mara baada ya kuwasili nchini.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Amerika na Ulaya Bw. Jestas Nyamanga naye akisalimia na "Prince" William mara baada ya kuwasili nchini. 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.