Follow by Email

Wednesday, August 15, 2018

Ubalozi wa Tanzania nchini Korea waandaa kongamano kuhamasisha wawekezaji sekta ya afya

Mgeni Rasmi katika Kongamano la kuhamasisha uwekezaji katika viwanda vya madawa na vifaa tiba nchini Bw. Geoffrey Mwambe, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji (TIC) akitoa hotuba ya ufunguzi, kwa niaba ya Mhe. Ummy Ally Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto, wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.   

Picha ya pamoja meza kuu: Kutoka kushoto: Makamu Mwenyekiti wa Korea-Africa Foundation (KAF), Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Geoffrey Mwambe, Balozi wa Tanzania Korea Mhe. Matilda Swilla Masuka, “Congressman” KIM Gyu-hwan, Rais wa KAF, Balozi Yeon-ho CHOI, na mwisho kulia ni Katibu Mtendaji wa Chama cha watengenezaji madawa (TAPI), Bw. Abbasi S. Mohamed.

Balozi wa Tanzania nchini Korea Kusini, Mhe. Matilda Swilla Masuka akitoa neno la ukaribisho katika Kongamano hilo.


Rais wa “Korea-Africa Foundation” waandaaji wenza wa Kongamano hilo, Balozi CHOI, Yeon-ho, akitoa neno katika hafla ya ufunguzi.


“Congressman” na Katibu wa “National Assembly Forum for Africa’s New Era” katika Bunge la Jamhuri ya Korea, Mhe. KIM, Gyu-hwan akitoa salamu za pongezi katika Kongamano hilo.  

 
Picha ya Pamoja ikijumuisha meza kuu na watoa mada kutoka: TIC, TFDA, MSD, Korea Health Industry Development Institute (KHIDI) na “Korea Medical Devices Industrial Association”.

Add caption

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bw. Geoffrey Mwambe ulipokutana na Kampuni ya LS watengenezaji wakubwa wa Matrekta na vifaa vya kilimo nchini Korea Kusini wenye lengo la kupanua wigo wa biashara kwa kuwa na uwakilishi na pia kuwekeza kwenye kiwanda “Assembly Plant”. 

Sehemu ya ujumbe kutoka Tanzania wakiwa na mwenyeji wao Balozi Matilda Swilla Masuka, baada ya kufanikisha Kongamano hilo la aina yake na lililovutia makampuni ya madawa na vifaa tiba zaidi ya 100.

Ujumbe kutoka Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Wana Diaspora ambao walishiriki kikamilifu katika Kongamano hilo la kuhamasisha wawekezaji katika viwanda vya madawa na vifaa tiba.

Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bw. Geoffrey Mwambe, ulipotembelea Kampuni ya kutengeneza Madawa ya Celltrion, na kujionea shughuli mbalimbali za kampuni hiyo. Celltrion ni kampuni maarufu na inashika Na.1 nchini Korea katika “ sekta ya Bio-pharmacy”. Wakati za ziara hiyo ujumbe wa Tanzania uliambatana na Balozi wa Tanzania Korea, Mhe. Matilda Swilla Masuka, na Rais wa “Korea-Afrika Foundation”, Balozi Yeon-ho CHOI

===================================================================
KONGAMANO LA BIASHARA NA UWEKEZAJI
KUHAMASISHA WADAU WA MADAWA NA VIFAA TIBA KUWEKEZA NCHINI TANZANIA LAFANYIKA SEOUL, KOREA

Ubalozi wa Tanzania uliopo Seoul nchini Korea kwa kushirikiana na “Korea-Africa Foundation” na “Korea Chamber of Commerce and Industry” uliandaa Kongamano la Biashara na Uwekezaji kwa wadau wa sekta ya Afya lililofanyika Seoul, Jamhuri ya Korea.  Kongamano hilo la aina yake, liliandaliwa ili kuunga mkono juhudi za Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuboresha sekta ya Afya.

Kongamano hilo lililenga kuhamasisha uanzishwaji wa viwanda vya madawa na vifaa tiba nchini Tanzania, lilihudhuriwa na makampuni zaidi ya 100, kutoka pande zote mbili ikijumuisha: Makampuni ya utengenezaji madawa na vifaa tiba; Vyuo Vikuu; Taasisi za utafiti; Hospitali; Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Makampuni kutoka katika sekta binafsi; na Diaspora wa Tanzania waliopo Seoul.


Wakati wa Kongamano hilo, mada mbalimbali ziliwasilishwa zikijumuisha: Fursa zilizopo Tanzania katika sekta ya utengenezaji wa madawa na vifaa tiba; Mazingira ya ufanyaji biashara na vivutio “incentives” vinavyotolewa na Serikali; Hali ya soko na uhitaji (Market Potentiality); Taratibu za kufuatwa katika uingizwaji wa bidhaa za madawa na uanzishwaji wa viwanda husika; na Utayari wa sekta binafsi katika kushirikiana na wenzao wa Korea katika biashara na ubia katika viwanda vya madawa na vifaa tiba.

Kongamano hilo lilijumuisha wadau kutoka Wizara na Taasisi za kuitendaji za hapa nchini ikiwa ni pamoja na  Wizara ya Afya; Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji; Kituo cha Uwekezaji (TIC); MSD; TFDA, na Chama cha wenye Viwanda vya Dawa Tanzania (Tanzania Association Pharmaceutical Industries-TAPI).


Kwa upande wa Korea wawakilishi walitoka  Vyama vya watengenezaji wa madawa na vifaa tiba walitoa mada iliyokuwa na lengo la kubadilishana uzoefu na upande wa Tanzania. Kongamano lilihitimishwa kwa B2B, ambapo makampuni na Taasisi zilikutana kujadiliana zaidi fursa, maeneo ya ushirikiano, na kupata ufafanuzi wa kina katika maeneo mbalimbali; na baadaye kutembelea Makampuni ya Madawa.       

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.