Follow by Email

Thursday, August 9, 2018

Rais Dkt. Magufuli afanya mazungumzo na Rais Museveni Ikulu jijini Dar es Salaam


Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya mazungumzo na Mhe. Yoweri Museveni Rais wa Jamhuri ya Uganda yaliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam.

 Rais Museveni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mashariki amefanya ziara ya siku moja ya kikazi nchini.

Rais Museveni akizungumza na wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Dkt. Magufuli, alieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kumpa taarifa Rais Magufuli kuhusu masuala yanayojiri kwenye mkutano wa BRICS uliofanyika Afrika Kusini.

Katika mkutano huo  ambao Afrika Mashariki ilishiriki kama kanda, Rais Museveni alitumia nafasi hiyo kuzishawishi nchi wanachama wa BRICS kuja kuwekeza Afrika Mashariki katika sekta za miundombinu ya uchukuzi na viwanda.

Aidha, Rais Museveni amempongeza Rais Magufuli kwa jitihada zake za kufufua Shirika la ndege la Tanzani ambalo litaleta mchango mkubwa katika kukuza utalii nchini. 

Mhe. Yoweri Museveni Rais wa Uganda akizumgumza na wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na mwenyeji wake Rais Mhe. Dkt John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam
Mhe. Yoweri Museveni Rais wa Uganda akisalimiana na baadhi ya watendaji wa Serikali waliojitokeza kumlaki wakati akiwasili uwanja wa ndege jijini Dar es SalaamMhe. Yoweri Museveni Rais wa Uganda  akiwa na mwenyeji wake Rais Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, akiwasalimia wananchi waliojitokeza kumpokea uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam

Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akijadili jambo na Mhe. Amelia Kyambade Waziri wa Biashara, Viwanda, na Ushirika wa Uganda  

Balozi Ramadhani Mwinyi Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia mkutano uliokuwa ukiendelea

Baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Serikali wakimuaga Rais Museveni wakati anaondoka uwanja wa ndege wa jijini Dar es Salaam kurejea nchini kwake

Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifurahi pamoja na wananchi waliojitokeza kumuaga Rais Museveni wa Uganda uwanja wa ndege jijini Dar es Salaam

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.