Follow by Email

Tuesday, August 14, 2018

Wajumbe wa Mauritius wa wasili nchini kuangalia maeneo ya Uwekezaji wa viwanda vya sukari.Ujumbe wa Serikali ya Mauritius ukiongozwa na Balozi wao mwenye Makazi yake Mjini Maputo, Msumbiji Mhe. Jean Pierre Jhumun umewasili nchini kwa ajili ya kukamilisha taratibu za uwekezaji wa viwanda vya sukari.

Ukiwa nchini, ujumbe huo umepanga kukutana na Viongozi mbalimbali wakiwemo;  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Waziri wa Kilimo, Waziri wa Mazingira (Ofisi ya Makamu wa Rais), Uongozi wa kituo cha Uwekezaji (TIC), Bodi ya Sukari pamoja na kuonana na Uongozi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Pichani, ni Balozi Jhumun (kushoto) na Bwana Gansam Boodram (kulia) , CEO wa Mauritius Sugar Board, pamoja Mhe. Balozi Ramadhan Mwinyi (kati) ambaye ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki

Aidha, Ujumbe huo unategemea kutembelea maeneo mbalimbali, ikiwemo mkoa wa Pwani, Wilaya ya Rufiji kwa ajili ya kuangalia maeneo ambayo wanategemea kuanza awamu ya kwanza ya uanzishaji wa kiwanda kikubwa cha kuzalisha sukari ambacho kinategemea zaidi ya wananchi 6000. 
Awamu ya pili ya Mradi huo (baada ya miaka mitano) inategemewa kufanyika Mkoani Kigoma ambapo sukari itakayozalishwa pia itasafirishwa na kuuzwa katika nchi za jirani.

Ziara hii inafuatia ombi la Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alilotoa (mwezi Marchi, 2017) kwa Mhe. Balozi Jhumun kumtaka kusaidia kuleta wawekezaji watakaoanzisha Viwanda vya sukari hapa nchini, wakati Balozi huyo akiwasilisha Hati za Utambulisho, Ikulu Dar es Salaam.
Kaimu Katibu Mkuu Mhe Balozi. Ramadhan Mwinyi akikaribisha wageni hao.


Pichani ni Wajumbe wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), pamoja na Balozi Jhumun akiwa na Bw. Boodram kutoka Mauritius (kulia, mwisho).

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.