Follow by Email

Sunday, July 8, 2018

Waziri Mahiga atembelea maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa (Sabasaba)Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akisaini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Wizara hiyo kwenye maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa yanayoendea katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.
Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (katikati) akisikiliza maelezo kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, alipotembelea banda la Wizara.

Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika mahojiano na wanahabari kwenye maonesho ya biashara kimataifa maarufa sabasaba yanayofanyika jijini Dar  es Salaam
Mhe.Waziri akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Wizara alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

Mhe. Mahiga akisikiliza maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara kwenye maonesho ya biashara ya kimataifa ya sabasabaMhe. Mahiga akiwa kwenye banda la kituo cha kumbi za mikutano cha kimataifa (AICC) kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba. Mbele yake ni baadhi ya watumishi wa kituo hicho.


Mhe. Mahiga akisalimiana na mmoja wa wafanyakazi wa Africafe alipotembelea banda la kampuni hiyo kwenye maonesho ya sabasaba 
Mhe. Mhiga akiwa katika picha ya pamoja na  baadhi wafanyakazi wa  AccessBank alipotembelea banda la benki hiyo kwenye maonesho ya sabasaba


Mhe. Mahiga akimsikiliza mmoja wa wawezeshaji katika banda la UN kwenye maonesho ya sabasaba
Mhe. Mahiga akikabidhiwa zawadi ya mchoro na Bibi Hoyce Temu kutoka Kitengo cha Mawasiliano cha Umoja wa Mataifa (UN). Waziri Mahiga alitembelea banda la UN kwenye maonesho ya sabasaba na kupata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini.

Mhe. Waziri Mahiga akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa UN alipotembelea banda la taasisi hiyo  kwenye maonesho ya sabasaba

Mhe. Waziri Mahiga akipata maelezo kuhusu bidhaa kutoka kwa mjasiriamali anayeshiriki maonesho ya sabasaba
Mhe. Mahiga akiangalia bidhaa za mjasiriamali anayeshiriki maonesho ya sabasaba alipotembelea banda lake
Mhe. Mahiga akiangalia bidhaa za wajariamali
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kupata elimu katika banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.