Follow by Email

Tuesday, July 3, 2018

Wananchi waendelea kujitokeza katika banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba


Mama Anna Mkapa Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, akiangalia moja ya machapisho yanayopatikana katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya biashara ya sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Wananchi wengi wameendelea kujitokeza kwenye banda la Wizara ili kuongeza  uelewa  juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara, ikiwemo namna Wizara inavyosimamia na kuteleza sera ya mambo ya nje ya nchi,  faida  na hatua mbalimbali za mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki lipo katika jengo la sabasaba hall.Wananchi  wote wanakaribishwa 
Maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto) wakizungumza na wananchi waliojitokeza kwenye banda la Wizara (kulia)Sehemu nyingine ya watumishi wa Wizara wakihudumia wananchi

Sehemu nyingine ya wananchi wakiuliza masuala mbalimbali kwa watumishi wa Wizara
Sehemu nyingine ya wananchi wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara

Sehemu nyingine ya wananchi wakipewa maelezo na mtumishi wa Wizara

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.