Follow by Email

Thursday, July 5, 2018

Naibu Waziri atembelea maonesho ya 42 ya biashara ya kimataifa (sabasaba)Mhe. Dkt. Susan Kolimba Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,  akisaini kitabu cha wageni kwenye banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

 Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga pamoja na watumishi wa Wizara. 

Dkt. Kolimba alifurahishwa na ushiriki wa Wizara  kwenye maonyesho ya sabasaba, ambapo aliwasisitiza watumishi wa Wizara kuendelea kutumia fursa hiyo kutoa elimu kwa umma kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara. 
 Mhe.Dkt. Kolimba akipata maelezo kutoka kwa Bi. Mindi Kasiga

Mhe. Dkt. Susan Kolimba akizungumza na watumishi alipotembelea banda la Wizara kwenye maonesho ya sabasaba

Mkurugenzi wa Masomo wa Chuo cha Diplomasia Prof. Watengere Kitojo  akizungumza na watumishi alipotembelea Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwenye maonesho ya sabasaba .
Wanafunzi kutoka Chuo cha Diplomasia wakipata maelezo kutoka kwa watumishi wa Wizara walipotembelea bandala kwenye maonesho ya saba.Wanafunzi hao walipata fursa ya kuelezwa kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda na kimataifa sambamba na fursa na faida zinazopatikana.
Bw. Teodos Komba Afisa Mawasilino, akielezea jambo kwa wananchi waliojitokeza  kwenye banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Bw. Hassan Mnondwa akielezea jambo kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara.

Mhe.Dkt. Susan Kolimba akiwa katika Picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alipotembelea banda la Wizara

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.