Follow by Email

Thursday, May 31, 2018

Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji wafikiatamati


Mhe. Mhandisi Stella Manyanya Naibu Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji akifuatilia Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji la Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea.

Mkutano huu ulilenga kujadili na kutolea ufumbuzi masuala mbalimbali yakiwemo ya kiforodha, ambayo yamekuwa kikwazo katika ufanyaji wa biashara za kuvuka mipaka katika Jumuiya.

Mkutano huu uliofanyika kuanzia tarehe 25 hadi 30 Mei, 2018 na ku
hudhuriwa na nchi zote wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki ulifikia tamati tarehe 30 Mei, 2018 jijini Arusha.
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akizungumza kwenye Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliofanyika jijini Arusha.
Kutoka kushoto ni Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji, na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji wakifuatilia mkutano


Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akifuatilia Mkutano

Maza Kuu ikiongoza Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji uliokuwa ukiendelea jijini Arusha
Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto) akisaini taarifa ya Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara,Viwanda,Fedha na Uwekezaji. Kushoto Bw. Eliah Chilangazi Afisa Biashara kutoka Wizara ya Biashara, Viwanda, na BiasharaProf. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (kushoto), Mhe. Mhandisi Stella Manyanya (Mb) Naibu Waziri wa Biashara, Viwanda na Uwekezaji (Katikati), na Bw. Benard Haule Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji (kulia) wakishauriana jambo


Prof. Adolf Mkenda Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mhe. Dkt. Pindi Chana Balozi wa Tanzania nchini Kenya wakifuatilia mkutano
Waheshimiwa Mawaziri, Mabalozi na Watendaji wa Serikali wa nchi wanachama za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya mkutano

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.