Follow by Email

Friday, May 4, 2018

Mkutano wa 8 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki wafikia tamati jijini Arusha

Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la masuala ya Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki umehitimishwa  leo tarehe 04 Aprili, 2018 jijini Arusha.

Mkutano huu uliofanyika kuanzia Aprili 28 hadi Mei 5, 2018, kabla ya kuhitimishwa ulitanguliwa na mikutano ngazi ya Wataalamu, ngazi ya Makatibu Wakuu, na hatimaye Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta.

Pamoja na mambo mengine lengo la Mkutano huu lilikuwa ni kufanya mambo yafuatayo:-
kupokea na kujadili taarifa ya hali ya utekelezaji wa maamuzi yaliyofanywa na Mkutano uliopita wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi;
Kupokea na kupitia taarifa ya Kamati ya Takwimu;
Kupokea na kujadili taarifa ya Kikosi kazi cha kuandaa muswada wa kuanzishwa kwa taasisi za Umoja wa Fedha wa Jumuiya ya Afrika Mashariki;
Kupokea na kujadili taarifa ya Kamati ya Masuala ya Fedha; na
Kujadili taarifa ya mapendekezo ya utekelezaji wa Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha, Mkutano huu umefanikiwa kupata ufumbuzi wa masuala kadhaa ya kichumi na fedha ambayo yanalenga kuboresha na kurahisisha mazingira ya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mhe. Dkt. Philip Mpango Waziri wa Fedha na Mipango akifuatilia Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hotel ya Four Points jijini Arusha.

Mkutano ukiwa unaendelea

Mhe.Dkt. Mpango akizungumza wakati wa Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika Hotel ya Four Points jijini Arusha
Bibi Judica Omari (kushoto) Kamishna Msaidizi wa Ushirikiano wa Kikanda, kutoka Wizara ya Fedha na Mipango Tanzania akizumgumza wakati Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta la Fedha na Uchumi ngazi ya Wataalamu. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Biashara, Uwekezaji, na Sekta za Uzalishaji Bw. Bernard Haule kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.


Sehemu ya wajumbe wakifuatilia Mkutano

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.