Follow by Email

Saturday, May 5, 2018

Balozi Dkt. Dau ashiriki kujadili zao la nazi nchini indonesia.

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Thailand, Philippines, Cambodia, Brunei, Laos pamoja na Indonesia Dkt. Ramadhani Kitwana Dau, leo akichangia mada  kwenye Kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi kwenye mji wa Gorontalo Indonesia 
Kongamano likiendelea
Mhe Dau amefanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo nchini Indonesi Dkt. Amran Sulaiman, katika mazungumzo yao yaliyojikita katika kushirikiana na kukuza sekta ya kilimo baina ya Tanzania na Indonesia.

********************* 

Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Thailand, Philippines, Cambodia, Brunei, Laos pamoja na Indonesia Mhe Dkt Ramadhani Kitwana Dau, leo ameshiriki  katika Kongamano la Kitaifa kujadili zao la nazi kwenye mji wa Gorontalo Indonesia .
Balozi Dau alishiriki kwenye mjadala huo (panellist) kwa kutoa historia ya zao la nazi Tanzania ikiwemo uzalishaji na changamoto zake. Mkutano huo wa siku 2 umeanza leo na unashirikisha Wadau wote wa zao la nazi nchini Indonesia. Indonesia inaongoza katika uzalishaji wa nazi Duniani kwa kulima hekta 3.6 milioni na kuzalisha nazi zaidi ya tani 17 milioni. Kwa upande wake, Tanzania inaongoza kwa zao hilo Barani Afrika lakini inalima hekta 350,000. 
Zao la nazi kwa sasa linaongoza kwa bei kwenye soko la Dunia na kulipita zao la chikichi na hata mafuta ya Petroli . Nchini Indonesia mnazi mmoja unatoa kati ya nazi 100 hadi 150 ingawa wastani wa kitaifa Ni nazi 70 kwa mnazi mmoja. 

Aidha katika mkutano huo Balozi Dau alipata fursa ya kuzungumza na Waziri wa Kilimo wa Indonesia Mhe Dr Amran Sulaiman ambapo walikubaliana kukuza zaidi ushirikiano kwenye kilimo baina ya nchi hizi mbili. 

Pamoja na zao la nazi, Indonesia inaongoza Duniani kwenye mazao  kadhaa yakiwemo muhogo, Mahindi ya njano. 
Balozi Dau anatarajia kukutana na wawekezaji wa sukari michikichi na mihogo kwa madhumuni ya kuwashawishi kuja kuwekeza Tanzania .


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.