Follow by Email

Tuesday, April 10, 2018

Naibu Waziri akutana na kufanya mazungumzo na Mabalozi

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Susan Kolimba (kulia) akiwa katika mazungumzo na Mhe. Balozi Lt. Jen Wynjones Matthew aliyekuwa akihudumu Ubalozi wa Tanzania Moscow, Urusi. Mhe. Balozi Matthew amerejea nchini baada ya kumaliza muda wake. Mhe. Naibu Waziri amekutana na Mabalozi hao Ofisini kwake mjini Dodoma ambapo walijadili masuala mbalimbali ya namna kudumisha uhusiano wa kidiplomasia na nchi husika ambazo Mabalozi hao wanaiwakilisha nchi, sambamba na kuibua maeneo mapya ya ushirikiano na nchi hizo.

Naibu Waziri Mhe.Dkt. Kolimba akiwa katika mazungumzo na Mabalozi wanaotarajia kwenda kuripoti kwenye vituo vyao vya uwakilishi hivi karibuni. Kulia ni Inspekta Jenerali mstaafu Mhe. Balozi Ernest Jumbe Mangu anayetarajiwa kwenda kuiwakilisha Tanzania Kigali, Rwanda hivi karibuni na kushoto ni Meja Jenerali Mstaafu Mhe. Balozi Mumwi Simoni anayekwenda kuiwalisha Tanzania Moscow,Urusi

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.