Follow by Email

Tuesday, January 23, 2018

Timu Maalum ya ADB yatembelea TanzaniaKatibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda (kulia) akiwa katika mazungumzo na Bw. Alieu Jeng- Mjumbe wa Timu kutoka Bank ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank), walipomtembelea Wizarani tarehe 22 Januari,2018
Timu hiyo yenye jumla ya wajumbe watatu ambao watakuwa nchini kwa lengo la kujadiliana na Serikali kuhusu maeneo ya vipaombele ambayo wanaweza kusaidia kupitia bajeti yao ya 2018/2019. wakiwa nchini watakutana na Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Kwa mujibu wa wajumbe hao, bajeti hii itazingatia zaidi kusaidia Serikali kupitia maeneo  ya vipaombele yaliyoanishwa  ili kuwezesha Sekta binafsi kuweza kuchochea uchumi wa nchi kupitia biashara na Uwekezaji katika maeneo mbalimbali.  wajumbe hao waliwasili tarehe 14 Januari, 2018 na wanatarajiwa kuondoka tarehe 27 Januari,2018.


 Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Aldof Mkenda (kulia), akiendelea na mazungumzo na wajumbe wa Timu kutoka ADB ambao ni Bw.Alieu Jeng(Kushoto), Bw. Frsncois Nkulikiyimfura anayefuata na mwisho kushoto ni Bi.Eline Okuozeto

Katibu Mkuu, timu ya ADB na Wataalam kutoka Wizarani wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mazungumzo
No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.