Follow by Email

Wednesday, December 13, 2017

TANZIA


TANZIA

Marehemu Mama Badriya Kiondo
Familia za Bw. Kiondo wa Kwaminchi Tanga na Bw. Ramadhan Haji wa Betras, Zanzibar wanasikitika kutangaza kifo cha Mtoto wao mpendwa, Bi. Badriya Ramadhan Kiondo aliyekuwa Mkuu wa Utawala na Fedha katika Ubalozi wa Tanzania nchini India kilichotokea tarehe 11 Desemba, 2017 katika Hospitali ya Apollo mjini New Delhi, India. 

Mwili wa Marehemu Mama Kiondo unatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi tarehe 14 Desemba, 2017 saa 8.45 mchana kwa Ndege ya Shirika la Emirates. Aidha, mazishi yatafanyika katika Makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam Ijumaa tarehe 15 Desemba, 2017 saa 10.00 jioni.

Msiba wa Marehemu Mama Kiondo upo nyumbani kwa mumewe Bw. Frank Mwamkai Kiondo maeneo ya Ada Estate, Na. 73, Kinondoni, Barabara ya Ali Hassan Mwinyi karibu na Ubalozi wa Ufaransa.

Habari ziwafikie ndugu, jamaa na marafiki wote wa familia hizi popote pale walipo.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. AminaRATIBA YA MAZISHI YA MAREHEMU BI. BADRIYA RAMADHAN KIONDO
No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.