Follow by Email

Thursday, June 15, 2017

TANGAZO KWA UMMA

TAARIFA KUHUSU KUTHIBITISHA VYETI


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma ya kwamba, wale wote wanaohitaji na watakaohitaji kupata huduma ya kuthibitisha vyeti na nyaraka mbalimbali kama ifuatavyo:

(1)  KuanziaTarehe 01/07/2017 malipo yote ya huduma ya kuthibitisha vyeti/nyaraka yatafanyika kwa njia ya benki, kupitia akaunti namba 0150275408200, Foreign Collection Account, CRDB Bank na hati ya malipo ya benki iwasilishwe wizarani kuthibitisha malipo hayo.

(2)  Wizara haitapokea pesa taslimu kama ilivyokuwa inafanyika hapo awali bali hati ya malipo kutoka benki.Kila nakala itakayothibitishwa na kugongwa muhuri italipiwa kiasi cha Shillingi Elfu Kumi na Tano tu (TSHS 15,000/=) benki.

(3)  Vyeti vyote vinavyoletwa Wizarani kwa ajili ya kuthibitishwa, havinabudi kupelekwa kwanza katika Taasisi zilizotoa vyeti/nyaraka hizo ili vihakikiwe na kuthibitshwa.

(4)  Baada ya kutekeleza maelekezo katikak ifungu cha tatu (3) hapo juu, Mteja anatakiwa kuandika barua kwa Katibu Mkuu,Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki akiomba nyaraka hizo zithibitishwe na kueleza matumizi tarajiwa ya nyaraka hizo nje ya nchi. Aidha, barua hiyo iambatishwe na nakala (copies) za nyaraka zilizothibitishwa na Taasisi husika.

(5)  WATEJA WOTE WANAOMBWA KUZINGATIA RAI KWAMBA HUDUMA HIZI ZITAKUWA ZINATOLEWA SIKU YA JUMANNE NA ALHAMISI TU, KUANZIA SAA 3.00 - 5.00 ASUBUHI.

Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.