Follow by Email

Thursday, April 13, 2017

Naibu Waziri Mambo ya Nje akutana na Balozi wa Italia nchini

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba (Mb) akizungumza na Balozi wa Italia nchini, Mhe. Roberto Mengoni alipomtembelea leo Wizarani Jijini Dar es Salaam. Mazungumzo yao yalijikita katika masuala ya ushirikiano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo mawili na hali halisi ya maendeleo katika sekta ya Elimu, Afya na Ujenzi wa Miundombinu.
Mhe. Mengoni akimweleza Naibu Waziri Kolimba nia ya dhati ya Serikali ya Italia katika kuongeza maeneo ya ushirikiano na Tanzania na kwamba inaunga mkono jitihada za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo. Pia alitumia fursa hiyo kupongeza hali ya amani iliyopo nchini na juhudi zinazofanywa katika kuhakikisha nchi jirani zinakuwa na amani.

Mazungumzo yakiendelea.
Mhe. Kolimba akiagana na Mhe. Mengoni.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.