Follow by Email

Monday, February 27, 2017

Wizara ya Mambo ya Nje yahamia Dodoma Rasmi


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Ofisini kwake Mjini Dodoma. Waziri Mahiga leo ameutangazia Umma wa Watanzania kuwa Wizara imehamia Dodoma rasmi.TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

KUHUSU WIZARA KUHAMIA DODOMA

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha Umma kuwa tayari imeshahamia Dodoma kuanzia tarehe 17 Februari, 2017.  Hatua hiyo imehusisha Awamu Mbili, awamu ya kwanza imetekelezwa tarehe 28 Januari, 2017 na awamu ya pili imetekelezwa tarehe 17 Februari, 2017.

Miongoni mwa Watumishi waliohamia Dodoma katika awamu hii ya kwanza ni pamoja na Viongozi Wakuu na Watumishi wa Wizara wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe.  Dkt. Augustine P. Mahiga na Naibu Waziri Mhe. Dkt. Susan A. Kolimba pamoja na Watumishi Kumi (10) waliofuatana nao.

Awamu ya pili iliongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara, Balozi Dkt. Aziz P. Mlima na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhan M. Mwinyi ambao waliongozana na Watumishi 33 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Katika Uhamisho huu, jumla ya Watumishi 43 wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wameungana na Viongozi wao Wakuu kwenye ofisi za Makao Makuu ya Wizara na Serikali Dodoma.

Mawasiliano ya Wizara yatakayotumika kuanzia sasa ni kama ifuatavyo:

Katibu Mkuu,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Barabara ya Makole,
S.L.P 2933,
Jengo la LAPF, Ghorofaya6,
DODOMA.

Namba za Simu: +255 (0) 262323201-7,
Nukushi           :  +255-26-2323208,
Barua pepe      :   nje@nje.go.tz
 Tovuti             : www.foreign.go.tz


Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma, 27 Februari, 2017.

Mhe. Waziri Mahiga na Naibu Katibu Mkuu Balozi Ramadhani Mwinyi wakijadili jambo kabla ya kuanza kwa mkutano Ofisini Mjini Dodoma.

Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri Mahiga kuhusu Wizara ya Mambo ya Nje kuhamia Dodoma.

Waziri Mhe. Balozi Dkt. Mahiga akiwa katika picha na baadhi ya watendaji wa Wizara mjini Dodoma. 
Walioketi ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (wa pili kulia), Naibu Katibu Mkuu,  Balozi Ramadhani Mwinyi (wa kwanza kulia) Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bw. Nigel Msangi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Bw.Hamid Mbegu wakiwa katika picha ya pamoja na  watumishi wa Wizara Mjini Dodoma. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.