Follow by Email

Friday, February 24, 2017

Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mhe. Samwel Shelukindo awasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Rais François Hollande jijini Paris leo


Mheshimiwa Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa akiwasilisha Hati zake za Utambulisho kwa Mheshimiwa François Hollande, Rais wa Jamhuri ya Ufaransa leo tarehe 23 Februari, 2017, Ikulu ya Ufaransa. Katikati ni Mheshimiwa Jean Marc Ayrault, Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa wa Ufaransa
Balozi Shelukindo akiwa kwenye mazungumzo rasmi na Mheshimiwa Rais François Hollande baada ya kuwasilisha hati zake za utambulisho.
Balozi Shelukindo na Mheshimiwa Hollande wakiendelea na mazungumzo kwenye Ikulu ya Ufaransa. Kulia kwa Mheshimiwa Hollande ni Waziri wa Mambo ya Nje na Maendeleo ya Kimataifa ya Ufaransa, Mheshimiwa Jean-Marc Ayrault na kulia kwa Balozi Shelukindo ni Bwana Stephen Wambura, Afisa Mambo ya Nje Mkuu na Kaimu Mkuu wa Utawala katika Ubalozi wa Tanzania mjini Paris.
Balozi Shelukindo akiagana na Mhe. Rais Hollande wa Ufaransa, baada ya kuwasilisha hati za utambulisho kwenye Ikulu ya nchi hiyo leo tarehe 23 Februari, 2017No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.