Follow by Email

Wednesday, November 30, 2016

Balozi Msechu apokea picha ya kuchora ya Rais Magufuli

Balozi wa Tanzania kwenye Nchi za Nordic na Baltic, Mhe. Dora Msechu amepokea picha ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kutoka kwa Msanii Mchoraji, Bw. Andrew Dudley Mliga nayeishi nchini Sweden.

 Bw. Mliga amesema kuwa alichukua uamuzi wa kuchora picha ya Mhe. Rais Magufuli baada ya kuhamasishwa  na kazi kubwa anayofanya  Mhe. Rais ya kuweletea maendeleo Watanzania. Ameeleza kuwa yeye ni miongoni mwa wanadiaspora wanaopata faraja kubwa kushuhudia jinsi  mafanikio ya uongozi wa Rais Magufuli  yanavyozidi kung'arisha  jina la Tanzania kwenye ramani ya Dunia.

Balozi Dora Msechu alipokea picha hiyo kwenye moja ya mikutano ya Jumuiya ya Watanzania wanaoishi nchini Sweden.

Bw. Mliga ni Msanii Mchoraji  anayeishi Sweden ambaye kazi zake zimejikita zaidi kwenye kuitangaza Tanzania kupitia fani ya uchoraji.
  Balozi Dora Msechu akipokea picha ya kuchorwa ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kutoka kwa Msanii Mchoraji, Bw. Andrew Dudley Mliga.       
picha ya kuchorwa ya Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli kutoka kwa Msanii Mchoraji, Bw. Andrew Dudley Mliga.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.