Follow by Email

Thursday, August 4, 2016

Waziri Mahiga apokea Nakala za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ireland nchini


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa amepokea Nakala za Hati za Utambulisho za Balozi Mteule wa Ireland nchini, Mhe.Paul Sherlock. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es salaam tarehe 04 Agosti, 2016
Mhe. Waziri Mahiga akizungumza ambapo alimkaribisha Mhe. Balozi Sherlock na kumweleza kuwa Tanzania na Ireland zimekuwa zikishirikiana vizuri tangu kuanzishwa kwa ushirikiano wa kidiplomasia baina yao na kwamba Serikali ya Tanzania itashirikiana na Balozi huyo katika muda wake wote wa uwakilishi hapa nchini.Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. James Bwana pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bi. Mona Mahecha walishiriki makabidhiano hayo.
 Mazungumzo yakiendelea

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.