Follow by Email

Wednesday, August 24, 2016

KONGAMANO LA WATANZANIA WANAOISHI UGHAIBUNI KUANZA LEO ZANZIBAR


Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Mindi Kasiga akizungumza na Wanahabari (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Katika Mkutano huo na Wanahabari Bi. Mindi Kasiga aliujulisha umma kuhusu kufanyika kwa Kongamano la siku mbili (24 -25 Agosti, 2016) la Watanzania wanaoishi Ughaibuni (Diaspora) linalotajiwa kuanza leo Mjini Unguja, Zanzibar.
Mmoja wa Watanzania anayeishi ughaibuni ambaye pia ni Mdau wa Michezo, Bw. Emmanuel Nasaa akizungumza na Wanahabari. Katika mazungumzo yake, Bw. Emmanuel Nasaa alielezea umuhimu wa Watanzania wanaoishi ughaibuni (Diaspora) kushiriki katika kuchangia jitihada za maendeleo nchini kupitia Sekta mbalimbali

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.