Follow by Email

Monday, June 13, 2016

Waziri Mahiga amuaga rasmi Balozi wa Italia hapa nchini.

 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), akimkabidhi zawadi Balozi wa Italia aliyemaliza muda wake wa uwakilishi hapa nchini, Mhe. Luigi Scotto, katika hafla maalumu ya kumuaga iliyofanyika tarehe 10-06-2016, kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb), akimkabidhi zawadi Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa Papa hapa nchini, Balozi Francisco Montecillo Padilla. Balozi Francisco alipewa zawadi hiyo kwenye hafla maalumu ya kumuaga Balozi wa Italia hapa nchini, iliyofanyika tarehe 10-06-2016, katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.

 Waziri Mahiga akifurahia jambo na Balozi Padilla na Balozi Scotto, mara tu baada ya kuwapa zawadi.
 Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa Papa hapa nchini, Balozi Francisco Montecillo Padilla (katikati), akizungumza jambo na Waziri Mahiga wakati wa hafla hiyo, huku Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki , Balozi Joseph Sokoine akifuatilia mazungumzo hayo.
 Ofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi. Olivia Maboko (kushoto) pamoja na Ofisa kutoka Ubalozi wa Italia hapa nchini, wakimsikiliza kwa makini Balozi Luigi Scotto (hayupo pichani), wakati akitoa neno la shukrani kwa Mhe. Waziri Mahiga.

 Maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bi.Robi Bwiru na Bw.Anthony Mtafya nao wakifuatilia hafla hiyo.
   .....hafla ikiendelea, huku wajumbe wakifurahia jambo.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga (Mb)(katikati), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Italia hapa nchini ambaye amemaliza muda wake wa uwakilishi, Balozi Luigi Scotto (kulia) pamoja na Balozi wa Vatcan na mwakilishi wa Papa hapa nchini, Mhe. Francisco Montecillo Padilla.
Picha ya pamoja na wajumbe wote waliohudhuria hafla hiyo.
=====================================
PICHA NA REUBEN MCHOME.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.