Follow by Email

Friday, June 17, 2016

Balozi Luvanda akutana na kufanya mazungumzo na Naibu Balozi wa Ujerumani

Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Baraka Luvanda (kulia), akizungumza na Naibu Balozi wa Ujerumani hapa nchini Bw. John Reyels ambaye alimtembelea hivi karibuni katika Ofisi za Wizara Jijini Dar es Salaam, ambapo katika mazungumzo yao walizungumzia juu ya kukuza na kuboresha mahusiano kati ya Tanzania na Ujerumani hasa katika sekta ya Biashara, Elimu na Uchumi.
Bw. Reyels katika mazungumzo yake aliipongeza Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, kwa juhudi zake katika mapambano dhidi ya rushwa.
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Luvanda na Naibu Balozi.
Mazungumzo yakiendelea
Picha ya pamoja 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.