Follow by Email

Tuesday, June 7, 2016

Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki atembelea Wizara ya Mambo ya Nje.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, Bi. Lilian Awinja. Bi. Awinja alionana na Katibu Mkuu kwa ajili ya kubadilishana mawazo kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo namna ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara la Afrika Mashariki, Bi. Lilian Awinja akisisitiza jambo wakati wa mazungumzo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima

Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Biashara, Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji, Bw. Bernard Haule, Mhandisi John Kiswaga, Msaidizi wa Katibu Mkuu na Bw. Elisha Suku kutoka Kitengo cha Sheria wakifuatilia na kunukuu mambo muhimu ya mazungumzo

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.