Follow by Email

Friday, March 11, 2016

Rais wa Vietnam amaliza ziara ya kitaifa ya siku nne nchini

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (kushoto) akiagana na Rais wa Vietnam  Mhe. Truong Tang San (wa pili kutoka kulia) mara baada ya kumaliza ziara yake ya siku 4 nchini.
Rais Truong Tang San (wa pili kushoto) pamoja na Mkewe Mai Thi akiagana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Augustine Mahiga (Mb.) mara baada ya kumaliza ziara yake hapa nchini.
Rais Truong Tang San akiagana pia na Balozi wa Tanzania nchini China ambaye pia anawakilisha Tanzania nchini Vietnam Mhe. Abdulrahman Shimbo.
Rais Truong Tang San akiagana na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australia wa Wizara ya mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Mbelwa Kairuki (wa kwanza kulia). 
Rais Tang San pia akiagana na Afisa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bw. Lwangisa
Rais Truong Tang San pamoja na Mke wake Bi. Mai Thi wakipunga mkono kwa pamoja kuwaaga viongozi wa Serikalini waliokuwepo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa kwa ajili ya kumuaga
Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (Mb.) (wa tatu kutoka kushoto), Waziri wa Mambo ya Nje Ushirikiano wa Kimataifa, Kikanda na Kimataifa Mhe. Augustine Mahiga (Mb.), Mkuu wa Mkoa wa Jiji la Dar Es Salaam Mhe. Said Meck Sadick (wa pili kutoka kushoto), Balozi wa Tanzania nchini China na anayeiwakilisha Tanzania nchini Vietnam Mhe. Shimbo wakipunga mkono kwa pamoja kumwaga Rais Tang San (hayupo pichani) na wa kwanza kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Bw. James Bwana  

Sehemu nyingine ya raia wa Vietnam wakiongozwa na Balozi wa Vietnam nchini Mhe. Vothanh Nam (wa tatu kutoka kulia) wakimwaga Mkuu wao wa nchi Rais Truong Tang San (hayupo pichani)
Viongozi wa Jeshi nao wakipiga saluti kwa kuashiria kumwaga Rais Tang San (hayupo pichani) mara baada ya kumaliza zaiara yake nchini Tanzania. 
Rais Tang San pamoja na Mke wake wakiwapungia mkono wananchi waliojitokeza kumwaga pamoja na kikundi cha ngoma kinavyoonekana pichani


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.