Follow by Email

Friday, March 11, 2016

Naibu Katibu Mkuu afanya mazungumzo na Balozi wa Ireland nchini


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Balozi Ramadhan Muombwa Mwinyi akizungumza na Balozi wa Ireland nchini Mhe. Fionnuala Gilsenan ambaye alimtembelea katika ofisi za Wizara na kuzungumza naye juu ya ushirikiano baina ya nchi hizi mbili hususan katika miradi ya Maendeleo inayohitaji kupewa kipaumbele katika Serikali ya Awamu ya Tano.
Mkurugenzi anayeshughulikia masuala ya Ushirikiano wa Afrika Magharibi na Mashariki kutoka Ireland, Bi. Emma Leonard kushoto ambaye aliambatana na Mhe. Balozi wa Ireland akifuatilia mazungumzo.
Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa,  Balozi Joseph Sokoine pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Anthony Mtafya wakifuatilia mazungumzo.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.