Follow by Email

Saturday, January 16, 2016

Waziri Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi wazungumza na waandishi wa Habari

Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akifanunua jambo kwa waandishi wa habari wakati akizungumza na waandishi hao Jijini Dar es Salaam, Kulia ni Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika ukumbi mdogo wa mikutano wa  Wizara, Jijini Dar es Salaam, Kushoto ni Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) alipomtembelea Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Augustine Mahiga (katikati), kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino  ya Serikali wa  Wizara ya Mambo Nje, Bi. Mindi Kasiga.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga (kulia) akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi, Mhe. Alain Aime Nyamitwe (kushoto) alipomtembea Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.