Follow by Email

Friday, January 15, 2016

Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na Mkurugenzi wa Kampuni ya Reli ya Malaysia

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Aziz Ponary Mlima (kulia) akimkaribisha Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya SMH-Rail kutoka Malaysia, Bw. S. Rajamohan, alipokutana nae na kufanya mazungumzo yaliyojikita katika uwekezaji katika sekta ya uchukuzi.
Bw. Rajamohan (kushoto) akizungumza huku Balozi  Mlima akimsikiliza
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga (Kushoto) na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Khatibu Makenga nao wakifuatilia kwa makini mazungumzo kati ya Balozi Mlima na Bw. Rajamohan (hawapo pichani).

Picha na Reginald Philip


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.