Follow by Email

Wednesday, December 9, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje na Siku ya Uhuru - 9 Desemba 2015

Tangazo la kurasa za Google Swahili mahsusi kwa siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2015. Kufuatia tamko la Mhe. Rais John Pombe Magufuli la kuadhimisha siku hiyo kwa kufanya usafi, Wakuu wa Idara na Vitengo wa Wizara ya Mambo ya nje wameshiriki kwenye zoezi la usafi kwenye maeneo ya makazi yao. Pia mabalozi wanaoziwakilisha nchi zaohapa wameitikia wito huo na kufanya usafi kwenye maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam. 

Balozi Liberata Mulamula, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa katika zoezi la usafi kwenye uzio wa nyumba yake maeneo ya Mbezi jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2015Nje ya uzio wa nyumba ya Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya kufanyiwa usafi kwenye maeneo ya Mbweni jijini Dar es salaam katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Desemba 2015.

Balozi Mohammed Juma Maharage, Mkuu wa Itifaki na Mkurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, akiwa kwenye zoezi la usafi kwenye gari maalum la "Rapid Deployment Unit" huko nyumbani kwake maeneo ya Makongo Juu, jijini Dar es salaam.


Mhe. Juma Khalfan Mpango, Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Kiongozi wa Mabalozi wa wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania naye akiwa kwenye zoezi la usafi nje ya ofisi za ubalozi maeneo ya Upanga jijini Dar es salaam. Usafi huo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru kufuatia maagizo ya Mhe. Rais John Pombe Magufuli ambapo kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni Uhuru na Kazi. 


Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa naye akisafisha maeneo ya pembezoni mwa bararabara kuu inayopita nyumbani kwake, Migombani maeneo ya Mikochini jijini Dar es salaam. 
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Mambo ya Nje Bi. Mindi Kasiga akisafisha ngazi za jengo la makazi yake Garden Avenue, jijini Dar es salaam ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru tarehe 9 Disemba 2015. 

Jumuiya ya Wachina wanaoishi hapa nchini wakifanya usafi kwenye maeneo yao ya kazi huku bendera ya nchi yako ikipepea ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara tarehe 9 Disemba 2015.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.