Follow by Email

Wednesday, November 11, 2015

Wizara ya Mambo ya Nje yamuaga rasmi Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini

Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula (kushoto), akimkabidhi picha ya kuchora kama zawadi ya ukumbusho kutoka Tanzania Balozi anayemaliza muda wa uwakilishi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Filiberto Sebregondi, katika hafla ya kumuaga iliyofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam tarehe 11 Novemba, 2015
Balozi Sebregondi akifurahia picha hiyo huku Mabalozi na Wageni waalikwa nao wakichukua picha za ukumbusho wa tukio hilo
Balozi Mulamula akitoa neno la shukrani kwa Balozi Sebregond, kwa niaba ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakati wa hafla hiyo
Sehemu ya Wageni waalikwa wakimsikiliza kwa makini wakati Balozi Mulamula (hayupo pichani) alipokuwa akitoa neno la shukrani
Balozi Mulamula akiendelea kuzungumza katika hafla hiyo
Balozi Filiberto Sebregondi naye alipata nafasi ya kutoa shukrani kwa ushirikiano aliokuwa akipata kutoka kwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Watanzania kwa ujumla wakati wa kutimiza majukumu yake akiwa kama mwakilishi wa Umoja wa Ulaya hapa nchini. 
Balozi Liberata Mulamula (kushoto) kwa pamoja na  Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo hapa nchini Mhe. Juma Mpango (katikati) na Naibu Katibu Mkuu  wa Wizara ya Fedha Dkt. Hamis Mwinyimvua (kulia) kwa pamoja wakimsikiliza Balozi Sebregondi (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga.
Maafisa Mambo ya Nje nao wakisikiliza kwa makini wakati Balozi Sebregondi (hayupo pichani) akizungumza. 
Balozi Mulamula na Balozi Sebregondi wakitakiana afya njema
Wageni waalikwa nao wakitakiana afya njema
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Mindi Kasiga akizungumza katika hafla ya kumuaga Balozi Sebregondi (hayupo pichani). 
Balozi Liberata Mulamula akiwa katika picha ya pamoja na Balozi anayewakilisha Umoja wa Ulaya hapa nchini Mhe. Filiberto Sebregondi
Picha ya pamoja.
 Picha na Reginald Philip.No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.