Follow by Email

Tuesday, November 17, 2015

Katibu Mkuu akutana kwa mazungumzo na wageni mbalimbali waliotembelea Wizarani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula akiwa katika mazungumzo na Mwakilishi Maalum wa Serikali ya China katika masuala ya Afrika, Balozi Zhong Jianhua alipotembelea Wizarani tarehe 17 Novemba, 2015.
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Samuel Shelukindo kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bw. Medard Ngaiza wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Balozi Zhong Jianhua (hawapo pichani)
Maafisa waliofuatana na Balozi Zhong Jianhua (hayupo pichani) nao wakifuatilia mazungumzo
Mazungumzo yakiendela...Mkutano wa Katibu Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari 


Balozi Mulamula (kulia) akizungumza na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Kuzuia Mauaji ya Kimbari, Bi. Felistas Mushi alipofika Wizarani kwa mazungumzo. 
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy kwa pamoja na Afisa Mambo ya Nje, Bi. Eva Ng'itu wakifuatilia mazungumzo kati ya Balozi Mulamula na Bi. Mushi (hawapo pichani)


Balozi Mulamula akiagana na Bi. Mushi baada ya mazungumzo yao


Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.