Follow by Email

Monday, October 5, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
 


Simu: 255-22-2114615, 211906-12
Barua pepe: nje@nje.go.tz
Barua pepe: gcu@nje.go.tz
Tovuti : www.foreign.go.tz     

Nukushi: 255-22-2116600

              

 

 
         20 KIVUKONI FRONT
P.O. BOX 9000,
      11466 DAR ES SALAAM, 
               Tanzania.

  


Taarifa zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa masikitiko makubwa imepokea jina la Bw. Khamis Juma Shamte hujaji kutoka Tanzania aliyefariki dunia kufuatia tukio la mkanyagano wa Mahujaji lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015. Kifo cha Bw. Shamte kinafanya idadi ya vifo vya Watanzania kufuatia tukio hilo kufikia watu nane (8) hadi sasa.

Aidha, Wizara imepokea jina la Bi Hawa Amrani Khamis aliyekuwa amepotea tangu siku ya ajali hiyo ambaye amepatikana akiwa mzima na aliweza kuungana na Mahujaji wengine na kurejea nyumbani tarehe 02 Oktoba, 2015.

Vile vile orodha ya majina ya majeruhi wote wa ajali ambao bado wapo hospitali imetolewa. Hadi sasa kuna Mahujaji wanne (4) wa Tanzania ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali mbalimbali za Saudi Arabia na hali zao zinaendelea vizuri. Mahujaji hao ni Bi. Hidaya Mchomvu, Bi. Mahjabin Taslim Khan na Bw. Ahmed Abdalla Jusab. Pia, kuna mgonjwa mmoja ambaye aliugua tangu alipowasili Madina akitokea nchini anayeitwa Mustafa Ali Mchira ambaye bado amelazwa katika Hospitali ya Ansari Madina katika chumba cha wagonjwa mahututi. Bw. Mchira hakujeruhiwa kwenye ajali ya mkanyagano.

Hadi kufikia tarehe 03 Oktoba, 2015, Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia kwa kushirikiana na Tanzania Hajj Mission na Vikundi vilivyopoteza Mahujaji umefanikiwa kupata majina ya Watanzania 32 ambao bado hawajapatikana. Orodha ya Majina na Vikundi vyao ni kama ifuatavyo:-

 KIKUNDI CHA KHIDMAT ISLAMIYA

1.  Abdul Iddi Hussein
2.  Awadh Saleh Magram
3.  Burhan Nzori Matata
4.  Yussuf Ismail Yussuf
5.  Saleh Mussa Said
6.  Adam Abdul Adam
7.  Archelous Anatory Rutayulungwa
8.  Farida Khatun Abdulghani
9.  Rashida Adam Abdul
10.              Hamida Ilyas Ibrahim
11.              Rehema Ausi Rubbaga
12.              Faiza Ahmed Omari
13.              Khadija Abdulkhalik Said
14.              Shabinamu Ismail Dinmohammed
15.              Salama Rajabu Mwamba
16.              Johari Mkesafiri Mwijage

KIKUNDI CHA TCDO

17.              Alwiya Sharrif Abdallah
18.              Hafsa Sharrif Saleh Abdallah

KIKUNDI CHA AHLU DAAWA

19.              Masoud Juma
20.              Issa Amiri Faki
21.              Juma Jecha Dabu
22.              Nassor Mohammed Hemed
23.              Mohammed Awadh Namongo
24.              Juma Yussuf Bajuka
25.              Said Habibu Ferej
26.              Khadija Hamad
27.              Rahma Salim
28.              Hadija Abdallah Sefu
29.              Farida Khamis
30.              Nuru Omar Karama
31.              Laila Manunga
32.              Saida Awadh

Zoezi la kuwatambua Mahujaji wa Tanzania ambao bado hawajaonekana linaendelea. Serikali ya Saudi Arabia imetoa picha nyingine zipatazo elfu moja (1,000) kwa ajili ya kuangalia Mahujaji waliofariki dunia katika ajali hiyo.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam

05 Oktoba, 2015

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.