Follow by Email

Friday, October 9, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARITaarifa zaidi ya Mahujaji kutoka Tanzania huko Saudi Arabia

Idadi ya mahujaji wa Tanzania waliopoteza maisha katika tukio la kukanyagana lililotokea eneo la Mina, Makkah tarehe 24 Septemba, 2015  imeongezeka kutoka 11 na kufikia 12 hadi sasa. Idadi hiyo imeongezeka kufuatia Bi. Aluiya Sharrif Saleh Abdallha kugundulika kuwa ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia katika tukio hilo. Bi. Abdallah alienda Makkah kufanya ibada ya hijjah kupitia kikundi cha TCDO.

Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Dar es Salaam
09 Oktoba, 2015

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.