Follow by Email

Friday, October 2, 2015

Balozi Marmo Afanya ziara ya Kikazi Mjini Hamburg

Mhe. Philip S. Marmo,Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani (Kushoto) akiwa kwenye kikao na Mhe.Wolfgang Schmidt, Naibu Waziri anaye shughulikia masuala ya Umoja wa Ulaya na Mambo ya Nje wa jimbo la Hamburg. Mkutano huo ulifanyika siku ya tarehe 29 Septemba,2015 kwenye ofisi Mhe.Schmdit mjini Hamburg.Mhe.Balozi Marmo alikuwa mjini Hamburg kwa ziara ya kikazi.
Mhe. Philip S. Marmo,Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani (wa kwanza kushoto) kwenye mazungumzo na Mhe.Vladimir Vladimirovich Golitsyn, Rais wa "International Tribunal for the Law of the Sea" aliyevaa tai ya zambarau (kulia) na Bi. Petra Hammelmann (katikati) Balozi wa Heshima wa Tanzania wa mji wa Hamburg. Mazungumzo hayo yalifanyika kwenye ofisi ya Mhe.Golitsyn siku ya tarehe 29 Septemba, 2015 mjini Hamburg.
Balozi Filip Marmo (wa pili kulia) akiwa katika Kaburi la Malika Salma Emily Ruete Binti binti wa Sultani Said Said wa Zanzibar ambaye alikuwa Mzanzibar wa KWanza kuja Hamburg mwaka 1866 na kuolewa na Mfanyabiashara wa Kijerumani. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.