Follow by Email

Wednesday, September 30, 2015

Tanzania yazindua rasmi Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu

Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Malengo ya  Maendeleo Endelevu  (SDGs), Naibu Katibu Mtendaji, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bw. Paul Kessy (kushoto) na Kamishna wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame (kulia). Uzinduzi huo  rasmi uliofanyika  hapa nchini katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam unafuatia uzinduzi uliofanywa na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Mataifa Mjini New York, Marekani tarehe 25/09/2015. Malengo hayo 17 ya miaka 15 yamerithi Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDGs) yaliyomaliza utekelezaji wake mwaka huu.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya MAmbo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya akiwa pamoja na baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka Mashirika ya Kimataifa na Balozi mbalimbali zilizopo nchini waliohudhuria uzinduzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu ( SDGs) iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa wawakilishi wa vijana akiuliza swali kuhusu utekelezaji wa Malengo hayo hapa nchini
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali na majibu.
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Bi. Joyce Mends-Cole naye akijibu moja ya swali lililoulizwa wakati wa uzinduzi wa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahya (wa pili kushoto) akiwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini, Bw. Alvaro Rodriguez (kulia), Kamishna wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame ( wa pili kulia) na Balozi wa  Ireland nchini , Mhe. Fionnuala Gilsenan (kushoto)  kwa pamoja wakifunua pazia maalum kuashiria uzinduzi rasmi wa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu  ( SDGs).
Wakishangilia baada ya kuzindua rasmi Malengo hayo hapa nchini.
Shamra shamra za uzinduzi zikiendelea. 
Mabalozi, Viongozi wa Serikali, Waandishi wa Habari na baadhi ya wanafunzi kutoka Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko  wakiwa kwenye picha ya pamoja huku wakiinua juu vibao vilivyoandikwa Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu  ( SDGs). Malengo hayo ni pamoja na Kuondokana na Umaskini;Kuondokana na Njaa; Kuondokana na Magonjwa; Kutunza na kuhifadhi Mazingira; Elimu Bora; Usawa wa Kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana; Huduma Bora za Jamii ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama;kukuza uchumi na kuongeza ajira; kupambana na mabadiliko ya tabianchi na upatikanaji wa nishati endelevu.
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Uhuru Mchangayiko walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha jamii kuhusu Malengo 17 ya Maendeleo Endelevu  ( SDGs).
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.