Follow by Email

Monday, September 14, 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Balozi Mteule Victoria Richard Mwakasege
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Ndugu Victoria Richard Mwakasege kuwa Balozi wa Tanzania nchini Malawi. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mwakasege alikuwa Naibu Balozi wa Tanzania nchini Burundi.    


Balozi Samwel Shelukindo

 Aidha, Rais Kikwete amemteua Msaidizi wa Rais wa Diplomasia, Balozi Samwel Shelukindo kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje naUshirikiano wa Kimataifa

Balozi Mteule Zuhura Bundala
Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) Balozi Ombeni Y. Sefue pia imesema kuwa Rais Kikwete ameteua Ndugu Zuhura Bundala kuwa Balozi na Msaidizi wa Rais (Diplomasia) kujaza nafasi iliyoachwa na Ndugu Shelukindo. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Bundala alikuwa Mkurugenzi Msaidizi na Kaimu Mkurugenzi, Idara ya Afrika. Balozi Mteule Abdallah Kilima
Taarifa hiyo iliyotolewa leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015, imesema vile vile kuwa Rais Kikwete amewateua wakurugenzi wengine wanne wa Wizara hiyo ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Kimatiafa na kuwapandisha cheo kuwa mabalozi.

Walioteuliwa ni Ndugu Abdallah Kilima ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Kilima alikuwa Afisa Ubalozi Mkuu, Ubalozi wa Tanzania, Muscat, Oman.

Balozi Mteule Baraka H. Luvanda

Ndugu Baraka H. Luvanda ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria. Kabla ya uteuzi  wake, Ndugu Luvanda alikuwa Mratibu wa Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi, Ikulu.Balozi Mteule Innocent E. Shiyo
Ndugu Innocent E. Shiyo ambaye anakuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kikanda. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Shiyo alikuwa Mkurugenzi Msaidizi katika Idara hiyo hiyo.Balozi Mteule Anisa K. Mbega


Bibi Anisa K. Mbega ambaye ameteuliwa kuwa Balozi na Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora. Kabla ya uteuzi wake, Ndugu Mbega alikuwa Mkurugenzi Msaidizi, Ubalozi wa Tanzania, Kampala, Uganda.


Uteuzi huo wote umeanza leo, Jumatatu, Septemba 14, 2015.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

14 Septemba, 2015


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.