Follow by Email

Wednesday, September 30, 2015

Mkurugenzi wa Asia na Australasia na Balozi wa India wajadili maandalizi ya India- Africa Summit

Mkurugenzi wa Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa Kairuki (kulia) akiwa katika mazungumzo na Balozi wa India nchini, Mhe. Sandeep Arya. Mazungumzo yao yalihusu pamoja na mambo mengine, ushiriki wa Serikali ya Tanzania katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi wa Kiafrika na India utakaofanyika jijini New Delhi, India tarehe 26 - 29 Oktoba 2015.

Mazungumzo kati ya Balozi wa India na Balozi Kairuki yanaendelea. Wengine katika picha, kulia ni Bw. Emmanuel Luangisa, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na kushoto ni Afisa wa Ubalozi wa India wakifuatilia mazungumzo hayo.


Balozi wa India nchini, Mhe.Sandeep  Arya akiagana na Balozi Kairuki mara baada ya kukamilisha mazunguzmo yao yaliyofanyika katika Ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.