Follow by Email

Friday, August 14, 2015

Naibu Waziri Mambo ya Nje aongoza ujumbe wa Tanzania Mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC

Dkt. Stagomena Tax, Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC akitoa hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Mawaziri wa jumuiya hiyo.

Picha ya pamoja ya Mawaziri waliohudhuria Kikao cha Baraza la Mawazi wa Nchi wanachanama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC, Jijini Gaborone, Botswana tarehe 14-15 Agosti, 2015


Mhe. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa kwenye ufunguzi wa Kikao cha Baraza la Mawaziri wa  Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) Jijini Gaborone, Botswana Ijumaa Agosti 14, 2015.

Ujumbe wa Tanzania kwenye Kikao cha Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya SADC uliiongozwa na Mhe. Mahadhi J. Maalim, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje (wa pili kulia), akifuatiwa na Balozi Simba Yahya, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje. Wengine mstari wa mbele ni Bw. Musa Uledi, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara (wa pili kushoto) na Dkt. Hamis Mwinyimvua, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha. 


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.