Follow by Email

Friday, August 28, 2015

Mkoa wa Kigoma kunufaika na Umeme wa nishati ya jua wa MW 5


Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Liberata Mulamula  akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya NextGen Solawazi Ltd ya kutoka Marekani, Bw. Mayank Bhargava. Katika mazungumzo hayo ambayo yalifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Bhargava alimjulisha Balozi Mulamula kuwa kampuni hiyo imeshaanza kazi ya kufunga mitambo ya kuzalisha umeme wa nishati ya jua wa MW 5 kwa ajili ya mkoa wa Kigoma. Aidha, alitoa taarifa kuwa hivi karibuni kampuni hiyo itaanza mchakato wa kufunga umeme wa nishati ya jua wa MW 16 kwa ajili ya mkoa wa Shinyanga.Bw. Bhargava akisisitiza jambo huku Balozi Mulamula akisikiliza kwa makini. Wa kwanza kushoto ni Bw. Cyril Batalia ambaye ni Mshauri Mwelekezi wa Kampuni ya NextGen Solawazi Ltd.


mazungumzo yakiendelea.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.