Follow by Email

Wednesday, July 1, 2015

Waziri Mkuu wa Ethiopia awasili nchini kwa ziara ya kikazi

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mizengo Peter Pinda (kulia) akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn (Katikati) mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Mhe. Desalegn yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili ambapo pamoja na mambo mengine atashiriki uzinduzi wa Kiwanda cha Viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria.
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn akisalimiana na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam
Waziri Mkuu, Mhe. Pinda akimtambulisha Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz kwa Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn.
 Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn. akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bi. Zuhura Bundala
Afisa Mambo ya Nje, Bw. Mudrick Soraga naye akisalimian na Mhe. Desalegn 
Waziri Mkuu wa Ethiopia akikagua Gwaride la Heshima mara baada ya kuwasili huku akisindikizwa na Mhe. Pinda
Waziri Mkuu wa Ethiopia, Mhe. Desalegn kwa pamoja na Mhe. Pinda wakimsikiliza Mhe. Membe wakati wa mazungumzo mafupi mara baada ya Mhe. Desalegn kuwasili.


............Matukio zaidi ya ziara ya Waziri Mkuu wa Ethiopia nchini

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Mhe. Desalegn, Mhe. Pinda na Bi. Joyce Phumaphi, Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Viongozi wa Afrika walio mstari wa mbele katika  kupambana na Malaria  (ALMA). Mhe. Desalegn ndiye Mwenyekiti wa sasa wa Taasisi hiyo wakati wa hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa Ikulu kwa heshima ya Mhe. Desalegn.
Balozi wa Cuba (kushoto), Mhe. Jorge Luis Lopez Tormo akiwa pamoja na Mkurugenzi  wa Idara ya Ulaya na Amerika, Balozi Joseph Sokoine (wa pili kushoto), wakimsikiliza Mkurugenzi na Mkuu wa Itifaki, Balozi Juma Maharage wakati wa hafla ya chakula cha jioni kwa heshima ya Waziri Mkuu wa Ethiopia.
Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Mhe. Naimi Aziz (mwenye kitambaa kichwani) akiwa na Kaimu Mkurugenzi  wa Idara ya  Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Bi. Zuhura Bundala pamoja na wageni wengine waalikwa wakati wa hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa Ikulu kwa heshima ya Waziri Mkuu wa Ethiopia.

Picha na Reginald Philip

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.