Follow by Email

Friday, May 22, 2015

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,  Balozi Mbelwa Kairuki (Kulia) akimkaribisha na kufanya mzazungumzo na Mkurugenzi wa Kitengo cha Afrika Mashariki katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Australia, Bi. Henderson. Mazungumzo yao yalijikita katika kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini hususani katika sekta ya Mafuta na Gesi.
Bi. Henderson akielezea jambo kwa Balozi Kairuki.
Wakwanza kushoto ni Bertha Makilage, (Katikati) ni   Bi. Zainabu Angovi, Maafisa Mambo ya Nje na kushoto ni Bi. Juliet Mutayoba ambaye yupo katika mafunzo  ya vitendo Wizara ya Mambo ya Nje.
Mazungumzo yakiendelea.
Picha ya Pamoja

Picha na Reginald Philip


MKUTANO NA BI. HENDERSON, MKURUGENZI WA KITENGO CHA AFRIKA MASHARIKI KATIKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA AUSTRALIA

Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia amekutana na kufanya mazungumzo na Bi. Henderson, Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Mashariki kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Australia leo tarehe 21 Mei 2015.

Katika mazungumzo yao, waligusia juu ya maendeleo ya maandalizi ya ziara ya Dkt. Kim Hames, Naibu Waziri Mkuu wa Jimbo la Magharibi mwa Australia na Waziri wa Afya na Utalii. Aidha Bi. Henderson aliipongeza Tanzania kwa kuandaa warsha na mikutano ya kutangaza fursa mbalimbali zipatikanazo nchini Tanzania ikiwa ni pamoja na  uwekezaji katika sekta ya mafuta, gesi na madini ambapo mwaka jana alihudhuria moja ya warsha iliyofanyika jijini Adelaide, Australia.

Kwa upande wake Balozi Kairuki alichukua fursa hiyo kuishukuru serikali ya Australia kwa nafasi za ufadhili wa masomo ya muda mfupi na mrefu katika sekta mbalimbali ikiwemo Kilimo na Afya.

Kwa kuhitimisha, Balozi Kairuki alimweleza Bi. Henderson juu ya uwepo wa fursa mbalimbali za uwekezaji nchini na kuwasihi wawekezaji kutoka Australia wasisite kuja kuwekeza katika sekta ya madini, nishati na gesi nchini.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.