Follow by Email

Wednesday, March 18, 2015

Waziri Membe amwakilisha Rais Kikwete, Lesotho


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wa katikati alipokuwa anaingia kwenye uwanja uliotumika kumwapisha Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Pakalitha Mosisili jijini Maseru jana. wengine katika picha, kutoka kulia ni Bibi Talha Mohammed, Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Mhe. Radhia Msuya, Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini ambaye pia anawakilisha Lesotho. kutoka kushoto ni Maafisa wa Serikali ya Lesotho.

Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Mosisili (kushoto) akikabidhiwa Bendera ya nchi hiyo na Waziri Mkuu wa Zamani, Mhe. Thom Thabane kama ishara ya kukabidhiwa rasmi madaraka ya uwaziri Mkuu.Waziri Mkuu mpya wa Lesotho, Mhe. Pakalitha Mosisiliakitoa neno la shukrani baada ya kuapishwa.
Viogozi mbalimbali wa Lesotho na kutoka nje ya Lesotho, mwenye kofia nyeupe ni mke wa mfalme wa Lesotho akiwa na mumewe ambaye ni Mfalme wa Lesotho.


Mandhari ya Uwanja livyokuwa wakati wa sherehe za uapisho.Waziri Membe (katikati) alipokuwa anawasili katika Uwanja wa Ndege wa Maseru kwa ajli ya kushiriki sherehe za uapisho. Mwingine ni Balozi wa Tanzania mchini Afrika Kusini, Mhe. Bibi Radhia Msuya.

Rais wa Afrika Kusini, Mhe. Jacob Zuma akiwasili Lesotho kwa ajili ya kushiriki sherehe za uapisho.

Rais Mteule wa Namibia, Mhe. Hage Geingob naye akiwasili Lesotho kwa ajili ya sherehe za uapisho.

Waziri Membe akihojiwa na Mwandishi wa Habari wa TBC, Bw. Stanley Ganzel mara baada ya sherehe kukamilika.Na Ally Kondo, Lesotho
Nchi za Afrika zimetakiwa kujifunza kutoka Lesotho, nchi ambayo dunia inashuhudia imekuwa na utaratibu wa kubadilishana madaraka kwa utulivu na amani bila fujo za aina yoyote. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) wakati wa sherehe za kumuapisha Waziri Mkuu mpya, Mhe. Pakalitha Mosisili zilizofanyika jijini Maseru siku ya Jumanne tarehe 17 Machi 2014. Waziri Membe alimwakilisha Rais Jakaya Kiwete katika sherehe hizo.

Mhe. Mosisili amerudi madarakani baada ya Chama chake cha Democratic Congress (DC) kuungana na vyama vingine sita vidogo kuunda Serikali ya Mseto. Mhe. Mosisili alikuwa Waziri Mkuu wa Lesotho kwa miaka 15 (1998 – 2012) na amerudi madarakani katika uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 28 Februari 2015. Uchaguzi huo ulifanyika mapema kwa miaka miwili kutokana na matatizo ya kisiasa yaliyosababisha kuvunjika kwa Serikali ya Mseto iliyokuwa inaongozwa na Waziri Mkuu wa Zamani, Mhe. Thom Thabane.

Katika hotuba yake, Mhe. Mosisili alisema kuwa nchi hiyo inakabiliwa na changamoto nyingi, hivyo, aliahidi kutumia uzoefu wake kuhakikisha kuwa nchi inaondokana na migogoro ya kisiasa ili iweze kusonga mbele kiuchumi.

Viongozi wengine waliohudhuria sherehe hizo ni pamoja na Rais wa Afrika Kusini,  Mhe. Jacob Zuma, Rais Mteule wa Namibia, Mhe. Hage Geingob na Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrka (SADC), Dkt. Stergomena Tax.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.