Follow by Email

Monday, March 16, 2015

WAZIRI MEMBE AKUTANA NA MTANZANIA ALIYESHINDA TUZO ZA COMMONWEALTH MJINI LONDON

Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa na Julius James Shirima, mshindi wa Tuzo ya Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola upande wa Afrika. Kwenye mazungumzo mafupi, Mhe. Membe alimpongeza Shirima kwa tuzo hizo na aliahidi kumpa ushirikiano kupitia Wizara anayoiongoza ili vijana wengi wa Kitanzania wanufaike na mchango wa Shirima na pia waige mfano wake na kuendelea kupeperusha vema bendera ya Tanzania.

Bw. Julius Shirima, mshindi wa Tuzo za Vijana wa nchi za Jumuiya ya Madola akiwa kwenye picha ya pamoja na Mhe. Bernard Membe, ambaye alifanya naye mazungumzo mara baada ya kumaliza kuendesha kikao cha Mawaziri wa Kikosi Kazi cha Jumuiya ya Madola mjini London hivi karibuni. Wengine kwenye picha ni Mhe. Peter Kallaghe, Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Bernard Membe, Julius Shirima, Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Balozi Celestine Mushy Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa. 

Julius James Shirima akiwa amebeba Siwa ya Jumuiya ya Madola ambapo aliongoza maandamano ya Malkia Elizabeth kwenye sherehe hizo kama mshindi wa Tuzo za Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola mwaka 2015. 

Malkia Elizabeth wa II, ambaye pia ni Mkuu wa Nchi 16 kati ya nchi 53 wanachama wa Jumuiya ya Madola akiwapongeza washindi Wanne wa Tuzo za Jumuiya ya Madola kutoka Afrika, Asia, Pacific na Karibian & Amerika, kabla ya kuzindua sherehe za Jumuiya hiyo mjini London, Uingereza. Pichani kulia ni Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Mhe. Kamalesh Sharma ambaye ndiye aliyekabidhi tuzo hizo kwa niaba ya malkia.


Washindi wa Tuzo za Vijana wa Nchi za Jumuiya ya Madola kwenye picha ya pamoja. Kutoka kushoto, majina yao na eneo waliloshindia kwenye mabano ni Bi. Brianna Frueann 16 wa Samoa (Pacific), Bw. Julius Shirima 26 (Afrika), Bi. Gulalai Ismael wa Pakistan (Asia) na Bi. Nolana Lynch wa Trinidad na Tobago (Caribbean & Americas) 


Bw. Julius Shirima akiwa nje ya Jengo la Jumuiya ya Madola Jijini London Uingereza wakati wa sherehe za jumuiya hiyo.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.