Follow by Email

Thursday, March 12, 2015

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola awasili London

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa Masuala ya Afrika wa Uingereza Mhe. James Duddridge baada ya kuwasili Jijini London kwa ajili ya kikao cha kazi cha Jumuiya ya Madola tarehe 11-12 Machi 2015.

Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akiwa na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola Mhe. Kamalesh Sharma kabla ya kuanza kikao cha faragha jijini London Uingereza leo.

Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Jijini London na kupokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe na Naibu Mkuu Mkuu wa Ubalozi Msafiri Marwa (wa pili kushoto) na Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Celestine Mushy.  
(Picha ya Juu na Chini) Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na ujumbe wake kwenye mazungumzo ya kikazi na Mhe. James Duddridge, Waziri wa Masuala ya Afrika wa Uingereza mara baada ya kuwasili London Jumatano tarehe 11/03/2015.(Picha ya Juu na Chini) Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na ujumbe wake wakiwa kwenye kikao cha kazi na Katibu Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Madola Mhe. Kamalesh Sharma Jumatano tarehe 11/03/2015.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.