Follow by Email

Thursday, February 12, 2015

Mhe. Rais Kikwete amwapisha rasmi Balozi HauleRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akimwapisha aliyekuwa  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Michael Haule kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya. Balozi John Michael Haule anachukua nafasi iliyoachwa  wazi na Balozi Batilda Buriani ambaye amehamishiwa Tokyo, Japan. Hafla hiyo ilifanyika Ikulu, Dar es Salaam tarehe 12 Februari, 2015
Balozi Haule akisaini kiapo chake mbele ya Mhe. Rais Kikwete
Mhe. Rais Kikwete akimkabidhi Balozi Haule vitendea kazi
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakishuhudia Balozi Haule (hayupo pichani) akila kiapo. Kulia ni Balozi Joseph Sokoine, Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika na Balozi Simba Yahya, Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati.
Balozi Yahya (mwenye tai nyekundu) kwa pamoja na Balozi Sokoine, Bi. Mindi Kasiga, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali na Bw. James Bwana (kulia), Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakifuatilia tukio la kuapishwa kwa Balozi Haule (hayupo pichani)

Bi. Zuhura Bundala (mwenye kilemba), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akiwa pamoja na Bibi Rosemary Jairo (mwenye suti nyeusi), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora wakifuatilia tukio la uapisho. Nyuma ya Bi. Bundala ni Bw. Nigel Msangi, Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu.
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Haule na Viongozi Wakuu wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal (wa tatu kushoto), Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda (wa nne kulia), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (kulia).
Mhe. Rais Kikwete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Haule na Mkewe
Mhe. Rais Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Haule pamoja na Waziri Membe, Naibu Waziri, Wakurugenzi na Wakuu wa Vitengo wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Mhe. Dkt. Mahadhi akisalimiana na Mama Haule mara baada ya Balozi Haule kuapishwa
Balozi Haule akipongezwa na Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia.
Balozi Haule akipongezwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukaguzi, Bw. Mathias Abisai
Balozi Haule akipongezwa na Mkuu wa Kitengo cha Uhasibu na Fedha katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Paul Kabale
Balozi Haule akipongezwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ununuzi na Ugavi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Balozi Haule akipongezwa na Katibu wa Waziri Membe, Bw. Thobias Makoba


Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha akimpokea na kumkaribisha Balozi Haule  Wizarani rasmi mara baada ya kuapishwa
Sehemu ya Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikinao wa Kimataifa wakimpokea kwa shangwe Balozi Haule mara baada ya kuapishwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Kenya
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Utawala, Bibi Amisa Mwakawago akimkabidhi maua Balozi Haule mara baada ya kuwasili Wizarani akitokea kuapishwa
Balozi Haule akiwashukuru baadhi ya Watumishi wa Wizara kwa mapokezi mazuri na ushirikiano
Baadhi ya Watumishi wa Wizara wakiwa na nyuso za furaha wakati wa mapokezi ya Balozi Haule (hayupo pichani)

Picha na Reginald PhilipNo comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.