Follow by Email

Friday, February 6, 2015

Katibu Mkuu John Haule, Balozi Mpya Nairobi, Kenya

Bw. John Michael Haule
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Bw. John Michael Haule, kuwa Balozi mpya wa Tanzania nchini Kenya.
Kabla ya uteuzi huu, Bw. Haule alikuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kuanzia mwaka 2011 hadi uteuzi huu.
Aidha, Rais Kikwete amemhamisha kituo Balozi Batilda Burian kutoka Nairobi, Kenya kwenda Tokyo, Japan kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Salome Sijaona ambaye anarejea nyumbani baada ya kustaafu.

Imetolewa na:

Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
05 Februari, 2015

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.