Follow by Email

Wednesday, January 14, 2015

Waziri Membe amuaga Balozi wa Algeria

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamiliusi Membe (Mb.) akimkabidhi zawadi ya picha yenye michoro ya Tembo  Balozi wa Algeria Mhe. Djelloul Tabel nchini Tanzania wakati wa hafla fupi ya kumuaga Balozi huyo ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini. Hafla hiyo ilifanyika Hyatt regency kempinski Hotel jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe (Mb.) akitoa neno la shukrani kwa Balozi wa Algeria Mhe.Djelloul Tabel, kwenye Hafla ya Chakula cha Mchana iliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Nje  kwa ajili ya kumuaga Balozi Tabel ambaye amemaliza muda wake wa kazi hapa nchini.

Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Afrika Bi. Zuhura Bundara akizungumza katika ghafla ya kumwaga balozi wa Algeria.
Balozi Djelloul Tabel akitoa neno la shukrani, wakati wa hafla ambapo alitoa shukrani kwa Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano aliopata katika kipindi chote alichokuwepo hapa nchini na kuomba ushirikiano huo uendelee.
Balozi Tabel akiendelea kuongea
Wageni waalikwa wakimpongeza Balozi Tabell kwa kumpigia makofi
Mkurugenzi Idara ya Asia na Australasia wizara ya Mambo ya Nje Balozi Mbelwa Kairuki naye akimsikiliza Balozi Tabell wa Algeria 


Waziri Membe akimweleza jambo Mhe. Balozi.
Waziri Membe wakigonga Glasi (Cheers)
Waziri Membe akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Algeria Mhe Tabell.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.