Follow by Email

Tuesday, January 13, 2015

Rais Kikwete awaandalia Sherry Party Wanadiplomasia wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Jakaya Mrisho Kikwete, akizungumza na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini katika hafla ya kuwatakia heri ya mwaka mpya, iliyofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam, Januari 9, 2015.
Baadhi ya Mabalozi wakimsikiliza Mhe. Rais katika hafla hiyo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe.Bernard Kamillius Membe (wa kwanza kulia) akiwa pamoja na maofisa wa wizara hiyo wakimsikiliza Mhe. Rais.
Mmoja wa mabalozi waliohudhuria hafla ya mwanzo wa mwaka akisalimiana na Mhe. Rais
Mmoja wa mabalozi waliohudhuria hafla hiyo,akisalimiana na Balozi Mbelwa Kairuki, Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa kimataifa Mhe.Bernard Kamillius Membe akiteta jambo na naibu wake, Mhe. Dkt.Mahadhi Juma Maalim na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Bw.John Haule (Kulia), wakisubiri kuanza kwa hafla ya mwanzo wa mwaka ya mabalozi.
Rais Kikwete (mstari wa mbele,katikati) akiwa katika picha ya pamoja na waheshimiwa mabalozi wa nchi mbalimbali aliowaandalia hafla ya kufungua mwaka. Kulia kwa Mhe. Rais ni waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Membe,na kushoto kwake ni Naibu waziri wa Mambo ya Nje, Mhe.Dkt.Mahadhi. 
(Picha na Reuben Mchome)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.