Follow by Email

Wednesday, January 21, 2015

Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje akutana na Ujumbe kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia


Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha (kulia) akisalimiana na Kansela Raffaele De Benedictis kutoka Wizard ya Mambo ya Nje ya Italia ambaye alifuatana na Balozi wa Italia nchini Tanzania Mhe. Luigi Scotto walipotembelea Wizara ya Mambo ya Nje leo.

Balozi wa Italia (katikati) akimtambulisha Kansela Benedictis kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia kwa Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, Balozi Rajabu Gamaha walipomtembelea ofisini kwake leo.

Balozi Gamaha (kulia) akiwa katika mazungumzo na Kansela Benedictis kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Italia. Wawili hao walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Italia, uwekezaji, usalama katika kanda pamoja na masuala ya kisiasa.

Mazungumzo yakiendelea. wengine katika mazungumzo hayo kutoka kushoto ni Balozi wa Italia, Mhe. Scotto, Kensela Benedictis, Balozi Gamaha, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi Victoria Mwakasege na Bibi Olivia Maboko, Afisa katika Wizara ya Mambo ya Nje.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.